Njia Za Kumfanya Mwenzi Wako Afurahie Kutumia Muda Na Wewe
1. KUWA NA AMANI
Watu wengi hujikuta wakirudi eneo lile linalowapata amani
2.KUTIMIZA MAHITAJI YA MWENZI WAKO
Wakati mwenzi wako ANAKUTIMIZIA mahitaji yako ya kimapenzi na ya kihisia lakini
anahakikisha umerizika, utaendelea kurudi kwake
3. KUWA MTU WA KUTHAMINI
Mshangilie mwenzi wako, onyesha kwamba unamthamini. Watu huenda mahali
wanaposherehekewa, sio kuvumiliwa tu
4. ONGEZA THAMANI YA MWENZI WAKO
Mwenzi wako anapokuwa na wewe, kuna wakati mwache aondoke akiwa yupo kwenye
ubora, mwenye busara, aliyeburudishwa zaidi, mwepesi, mwenye furaha zaidi
kuliko hapo awali. Kuwa mtu ambaye huongeza thamani kwa kusudi la mwenzi wako
na ubora
5. USIWE MTU WA KUHUKUMU KILA JAMBO
Epuka kuwa mtu wa kutoa kauli za kuhitimisha mapenzi yenu kama vile maneno haya
"Sikuzote unafanya hiki na kile" au kumtazama mwenzi wako kwa njia
tofauti anapofanya jambo ambalo haliendi sawa nawe au kuliingiza jambo
lisilopendeza kwenye mgogoro wenu. Watu wengi huepuka mazingira ya ugomvi na
kelele
6. KUWA MTU ROMANTIC
Jifunze jinsi ya kumgusa mwenzi wako, jinsi anavyopenda kuguswa. Mwenzi wako
ataendelea kuja kwako kwa ajili ya kuguswa tu
7. EPUKA UGOMVI
Jaribu kujiongoza hasa ukiwa na hasira, tambua jinsi ya kuharibu jazba. Sio
kila mnapogombana lazima mpigane.
8. USIWE MTU WA KULALAMIKA SANA NA KUTOA LAWAMA
Kosa ambalo wengi hufanya ni kuwashambulia na kuwalalamikia wenzi wao kwa jinsi
ambavyo hatengi muda wa kuwa na ampendae. Hii inasukuma mahusiano mbali badala
ya kuwa kivutio kwa mwenzi wako
9. ZUNGUMZIA KILE ANACHOPENDA
Jifunze mada zinazopendwa na mwenzi wako na ushiriki wa tendo. Itakuepusha kuwa
unamboa mpenzi wako
10. FURAHIA
Usipende kuchukulia maisha kwa uzito sana, tambua kuwa hewa hainyonywi na
hairambwi, usiwe na hasira. mJibu kwa utaratibu, kutaniana na tabia ya kucheza.
Burudani inakaribisha mapenzi
11. KUWA MSIKILIZAJI MWEMA
Watu huenda mahali kwaajili ya kusikika tu. Usitawale mazungumzo muda wote.
muonyeshe mwenzi wako mawazo yake, maoni na hadithi zake kuwa ni za muhimu
12. WASILIANA UNAPOMKOSA MWENZI WAKO
Mjulishe mwenzi wako jinsi nyinyi wawili mnavyokuwa na wakati mzuri mkiwa
pamoja. Itamfanya mwenzi wako ajisikie wa muhimu
13. MFANYE AWE ANAKUMISI
Unda hali ambayo mwenzi wako atataka kufurahiya uwepo wako, hali isiyo mbaya
kwa mwenzi wako atajaribu kukukwepa au hata kupita mahala ulipo ili akuone tu