Tuesday, April 29, 2025

Jinsi ya Kumsaidia Mume Wako - Kamata Elimu hapa

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 JINSI YA KUMSAIDIA MUME WAKO


Mke aliumbwa kama msaidizi na mwenzi. wewe huwa Unamsaidiaje?

1. Tafuta malengo yake ili uwe tegemeo lake

2. Wasiliana na malengo yako binafsi ili kwa pamoja mtimize kusudio lenu

3. Mpe Changamoto akue kiakili. lakin Usifurahie hali hiyo, mjulishe mawazo mapya juu ya jinsi ya kufanya ndoa yenu iende vizuri, jinsi ya kushughulikia fedha, jinsi ya kufanya kazi kwa busara, jinsi ya kuwa bora zaidi kwenu nyinyi wawili.

4. Yapendezeshe mazingira yake na kuyafurahisha macho yake. Kuna kitu cha kusisimua kuhusu mwanamke kwa mwanaume

5. Fanya kazi na uchangie kwenye mahitaji ya familia. Kuwa Mwanamke aliyetajwa kwenye Mithali 31. Wewe pia, ulienda shule, ulipewa agizo na mungu la kuzaa, kuzidisha, kujaza, kutiisha na kutawala. Iwe umeajiriwa au unafanya biashara, ongeza utajiri wa familia pamoja

6. Muonye juu ya hatari na usikubaliane naye anapokosea. Usiwe mwanamke wa kusema "Ndiyo" kila jambo juu ya maamuzi yake yote. Unaweza kuwa unayaona mambo na makosa ambayo yeye hayaoni

7. Mwombee na uwe pamoja naye. Mfunike kwa maombi

8. Kulea watoto pamoja naye. Unaweza kuwa na ujuzi tofauti wa wazazi lakini una malezi mazuri kwa watoto

9. Msikilize, kaa nae mahali ambapo anajisikia kuna usalama kuzungumza. Wanaume wengi wanateseka kimya kimya wakijiuliza waelekee wapi. Kwa wasiri wao

10. Mjenge. Usimwangushe kwa maneno yako. Usimshushie heshima, hiyo haisaidii

Add Comments


EmoticonEmoticon