Fanya haya ili Umuone Mpenzi wako ni Mpya kila Siku – Hutamchoka kabisa
Mwanamume na mwanamke wanapooana na kufanya ngono mara kwa mara, ni rahisi kujenga mazoea na kutengeneza njia ndogo za mapenzi na kufanya kila mtu kupunguza hamu kwa mwenzie na kumuona wa kawaida mpaka itokee siku mmoja kati yao awe na hamu ya tendo la ndoa. "Tayari mnapeana raha lakin za muda mfupi.
Ifuatayo ndiyo
njia halisi na halali na itakayokufaa ili usijenge mazoea na kumuona
mkeo/mpenzi wako wakawaida
1. Kumkumbatia mwenzi wako. ni Kitu rahisi sana japo watu wengi huchukulia
kawaida
2. Kumbusu mwenzi wako sehemu nyingi bila kuwekewa kizuizi na sehemu nyingine
za karibu kama midomo, paji la uso, mashavu, vidole, mgongo, shingo nk kamwe
usimuwekee mwenza wako vizuizi muache awe huru kwenye mwili wako muda wowote
mkiwa wote.
3. Kubembelezana na mwenzi wako pamoja na kuvaa mavazi ya kustrii mwili wako
kunaleta hamasa sana kwa mwanaume yeyote awe na hamu na wewe tafadhri usipende
kujiachia au kukaa uchi na kuonyesha maungo yako kwa mumeo mwanaume akikuona
mara nyingi ukiwa uchi huishiwa na hamu na kukfanya akuone wa kawaida.
4. Kushikana mikono na mwenzi wako hata kama kwa muda mfupi tu. ni kitu kizuri
sana huleta hamasa na kuamsha hisia
5. Kuminya mkono wa mwenzi wako huonyesha kujali, na kumfanya ajioneu kama
kwako ni mmoja, na mwenye upendo sana.
6. Jitahidi Kuusoma mwili wa mwenzi wako. Kuzingatia maeneo yake mengi ambayo
akiguswa au kuchezewa humpa hamu mfano kama kwa babu/bibi, na chuchu hiyo
itakusaidia.
7. Kumpongeza mwenzi wako akifanya jambo zuri zhumfanya ajione analindwa na
kujaliwa
8. Kukaa uchi mara kadhaa kwa pamoja, sio kwa sababu mnataka kupeana
michanganyo na minyongesho, bali ni kwa sababu mnataka kupeana raha na raha sio
mpaka tendo la ndoa mnaweza mkacheza tu chumbani huku mkifurahishana.
9. Wakati mwingine kula kwa kutumia bakuli/sahani moja. ni jambo la muhimu
chakula cha mumeo usiache aandae dada wa kazi
10. Kuangaliana, kuangalia movie pamoja na kubadirisha maeneo ya kupeana
michanganyo hii pia huleta hamu
11. Kutenga muda wa kuwa wa kuwa pamoja na kutofautisha nyakati za kuwa kwenye
mihangaiko ni mhimu sana.
12. kukaa chini na mwenzi wako Kuzungumzia kuhusu hisia zenu.
Ishara hizi unaweza kuona kama ndogo lakini zinaonyesha upendo kwa njia kubwa.